×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta asaini mswada unaowaweka wamiliki wa mikopo ya kidijitali kuwa chini ya udhibiti wa Banki Kuu ya Kenya CBK.

Rais Kenyatta asaini mswada unaowaweka wamiliki wa mikopo ya kidijitali kuwa chini ya udhibiti wa Banki Kuu ya Kenya CBK.

Rais Uhuru Kenyatta ametia saini miswada mitano ya bunge kuwa sheria.

Miswada iliyoidhinishwa na Rais kuwa sheria ni kama vile Mswada ya Ushirikiano wa Sekta za Umma na za Binafsi, Public Private Partnership Bill, Central Bank of Kenya Amendment Bill ule wa jopo la kushughulikia rufaa za masuala ya kodi, Tax Appeals Tribunal Amendment Bill.

Miswada mingine ni Mswada wa Washika-amana, Trustees Amendment Bill na Kenya Deposit Insurance Amendment Bill.

Mswada wa Central Bank of Kenya Amendment Bill, unawaweka wamiliki wa kampuni za kutoa mikopo ya kidijitali kuwa chini ya udhibiti wa Banki Kuu ya Kenya CBK.

 

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi na mwenzake wa Seneti Ken Lusaka, pamoja na Waziri wa Fedha Ukur Yatani na Mkuu wa Utumishi wa Umma Dkt Joseph Kinyua walihudhuria hafla hiyo fupi ya kutia saini.

Wengine walikuwapo ni Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Amos Kimunya na Wakili wa Serikali Ken Ogeto

Share this: