×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Polisi amuua mkewe na watu wengine watano kabla ya kujiuua mtaani Kangemi, Nairobi

Polisi amuua mkewe na watu wengine watano kabla ya kujiuua mtaani Kangemi, Nairobi

Polisi wamelazimika kutumia vitoza machozi kuwatawanya baadhi ya vijana waliokuwa wamefunga baadhi ya barabara kwenye mtaa wa Kangemi na Kabete na barabara ya Waiyaki wakilalamikia kuuliwa kwa wahudumu watatu wa bodaboda, na mmoja wa maafisa wa polisi ambaye alijiua baadaye.

Mvutano huo kati ya polisi na wahudumu wa bodaboda ulisababisha msongamano mkuwa wa magari baada ya barabara hizo kuzibw akwa mawe huku magurudumu yakiteketezwa.

Waliokuwa wakiandamana wanapinga kuuliwa kwa wahudumu hao wa bodaboda pamoja na majirani wawili waliofika nyumbani kwa afisa wa polisi kwa jina Benson Imbatu ambaye aliwaua watu 6 kabla ya kujiua akiwemo mkewe. Winfred Nyambura, ni mjane ambaye amempoteza mumewe aliyetambuliwa kwa jina Amos Njoroge.

<AUDIO>8003

Walioshuhudia mkasa huo wa mapema leo wamesema kwamba Imbatu mwenye cheo cha Konstable, alimuua kwanza mkewe kabla ya kuondoka chumbani na kuwafatualia risasi wapitanjia kiholela na kuwaua wengine watano kabla ya kujipiga risasi.

Taarifa ya wakazi ni tofuati na ya awali iliyodai kwamba waliopigwa risasi walikuwa wameenda katika makazi ya polisi huyo baada ya kusikia milio ya risasi.

Tayari maafisa wa polisi wamefika kuchukua mili ya waliouliwa na kuanzisha uchunguzi.

Share this: