×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Dereva aliyewashtaki wanafunzi kwa kuvuta bangi afutwa kazi

Dereva aliyewashtaki wanafunzi kwa kuvuta bangi afutwa kazi

John Muthoni, dereva wa gari la Kampuni ya 2NK Sacco, ameachishwa kazi kufuatia hatua yake ya kuwapeleka wanafunzi katika kituo cha polisi kwa madai ya kuvuta bangi.

Kampuni ya Uchukuzi ya 2NK imesema hatua ya dereva huyo ililenga kuharibu sifa za kampuni hiyo.

Muthoni mwenye umri wa miaka 32 alikuwa akiwasafirisha wanafunzi kumi na wanne kutoka Karatina, mjini Nyeri alipogundua kwamba wanafunzi hao walikuwa wakivuta bangi.

Kulingana na Muthoni, wanafunzi hao walianza kuvuta bangi wakiwa ndani ya gari ambapo juhudi zake za kuwaonya ziliambulia patupu.

Hali hivyo, ilimlazimu kuelekeza gari katika kituo cha polisi, huku wanafunzi wakiamua kutoroka kupitia dirishani ili kukwepa mkono wa sheria.

Haya yanajiri huku wanafunzi hao wakiendelea kutafutwa.

Wanafunzi hao ni wa Shule ya Upili ya Fred's Grammar Adventist Mukangu, Nyeri.

Muthoni anadai aliporejesha gari ofisini jioni, alipokonywa stakabadhi zote za kazi, huku akiagizwa kuondoka kwani uongozi wa 2NK Sacco haukuwa tayari kuhusishwa na kisa cha wanafunzi hao.

Kulingana naye uongozi wa 2NK SACCO haukumpa nafasi ya kujieleza, na badala yake kumkaripia kwa madai ya kulihabiria jina shirika zima.

Dereva huyo amesema katika shirika hilo, wafanyakazi hawasikizwi, na yeyote akipatikana katika kosa, anafurushwa bila uchunguzi kufanywa. Juhudi za kufikia uongozi wa 2NK zimekosa kuzaa matunda.

Haya yanajiri huku wanafunzi hao wakiendelea kutafutwa. Wanafunzi hao ni wa Shule ya Upili ya Fred's Grammar Adventist Mukangu, Nyeri.

Tayari mwalimu mkuu ameagizwa kufika katika Kituo cha polisi cha Sagana ili kusaidia katika kuwatambua wanafunzi hao kumi na wanne.

Share this: