×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Vijana 180, 000 wajisajili kujiunga na Kazi Mtaani katika muda wa saa 12

Vijana 180, 000 wajisajili kujiunga na Kazi Mtaani katika muda wa saa 12

Vijana elfu mia moja themanini na moja wamejisajili kujiunga na mpango wa kazi mtaani katika kipindi cha saa kumi na mbili zilizopita.

Kulingana na Katibu wa Wizara ya Nyumba Charles Hinga, vijana hao wamejisajili kupitia mfumo wa mtandao wa Kazi Mtaani, Management System KMS, katika shughuli iliyoanza hapo jana.

Hinga amesema Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa vijana elfu thelathini na saba na mia nane, ikifuatwa na Kiambu na elfu kumi na nne mia tisa kisha Nakuru na elfu tisa mia sita hamsini, ambao wamejitokeza kusajiliwa.

Hinga amewashauri vijana kujisajili katika mpango huo kwani wana muda wa wiki mbili zaidi.

Amewaonya walio na nia ya kuwalaghai vijana pesa kwa kuwahadaa kwamba watawapa kazi kupitai mpango huo.

Ikumbukwe serikali iliongeza muda wa mpango huo wa Kazi Mtaani hadi Juni mwaka ujao.

Mpango wa Kazi Mtaani unalenga kuwapa vijana ujuzi na uwezo wa kujisimamia kifedha.

Katika awamu ya kwanza takriban vijana elfu mia mbili themanini waliajiriwa katika maeneo elfu moja mia moja kwenye kaunti zote arubaini na saba.

Share this: