×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Askofu, Philip Anyolo atawazwa rasmi kuwa Mkuu wa Dayosisi ya Nairobi

Askofu, Philip Anyolo atawazwa rasmi kuwa Mkuu wa Dayosisi ya Nairobi

Hatimaye Askofu Philip Anyolo ametawazwa rasmi kuwa Mkuu wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Nairobi.

Hafla hiyo ambayo imefanyika katika Kanisa la St. Mary's Msongari hapa jijini Nairobi, imeongozwa na mwakilishi wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis humu nchini na Sudan Kusini Herbatus Maria Van Megan.

Akizungumza wakati wa misa ya kutawazwa kwakwa, Askofu Anyolo,  ameahidi kuendeleza ujumbe wa Kanisa Katoliki na kutoogopa kuzungumzia ukweli.

Askofu Anyolo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia masuala ya kitaifa kama vile uchaguzi mkuu wa mwaka ujao ambapo  ametoa wito kwa waliotwikwa jukumu la kuendesha shughuli hiyo kuhakikisha inaendeshwa kwa njia huru na haki.

Amepaza sauti yake kuhusu tatizo la uteketezaji wa majengo shuleni , tatizo la njaa na janga la korona akitoa wito kwa washikadau kuwajibika.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kadinali John Njue aliyekuwa Kiongozi wa Dayosisi ya Nairobi kabla ya kustaafu mapema mwaka huu, amemshauri Askofu Anyolo kushirikiana na waumini katika uongozi wake.

Anyolo atakuwa Askofu wa tano wa Dayosisi ya Nairobi.

Kabla ya uteuzi wake alikuwa Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Kisumu.

Kwa sasaa Askofu wa Dayosisi ya Nakuru Maurice Muhatia atachukua nafasi hiyo kwa muda kabla ya Askofu mwingine kuteuliwa na Papa Francis.

Share this: