×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto ashtumu kutimuliwa kwa Wycliffe Ogolla

Ruto ashtumu kutimuliwa kwa Wycliffe Ogolla

Naibu wa Rais, William Ruto ameelezea haja ya kuwajibishwa kwa Idara ya Polisi, NPS kufuatia misururu ya visa vya utovu wa usalama nchini.

Akihutubu kwenye eneo la Kionjokoma Kaunti ya Embu, Ruto ameanza kwa kuwapigia pole wakazi wa eneo hilo kufuatia kuuliwa kinyama kwa ndugu wawili, huku akiwahakikishia kwamba haki itapatikana.

Aidha, Ruto ameshtumu kutimuliwa kwa Mkuu wa Magereza, Wycliffe Ogallo kufuatia madai ya utepetevu kazini, hali iliyosababisha kutoroka kwa wafungwa watatu katika Gereza la Kamiti. Ruto ametaka Wizara ya Usalama wa Ndani ya Nchi kuwajibishwa ipasavyo.Kauli yake imetiliwa mkazo na wabunge Ndindi Nyoro wa Kiharu na Rigathi Gachagua wa Mathira ambao wamesema maafisa wadogo wadogo wanawajibishwa ilhali wakubwa wao wanasazwa.

Miongoni mwa walioandamana na Ruto ni Gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru ambaye licha ya kujizatiti kuelezea kuhusu mfumo wa kuwainua wananchi wenye kipato cha chini, bottom up economic model, wakazi walimpuuza.

Share this: