×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wafungwa watatu waliotoroka wakamatwa

Wafungwa watatu waliotoroka wakamatwa

Wafungwa watatu wa ugaidi Mohamed Ali Abikar, Joseph Juma Odhiambo na Musharaf Abdallah Washiali waliokuwa wametoroka katika Gereza la Kamiti wamerejeshwa gerezani humo ambapo wanatarajiwa kuongezewa mashtaka ya kutoroka jela. Watatu hao wamekamatwa kwenye msitu mmoja mpakani pa Kaunti za Tana River na Kitui, wakieleka Garissa kabla ya kuingia nchini Somalia.

Akizungumza wakati wa kuwarejesha Gerezani, Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai amesema wafungwa hao walilenga kuingia Somalia kupitia Msitu wa Boni uliopo mpakani pa Kenya na Somalia.

Wakati wa kikao hicho, Waziri wa Usalama Fred Matiang'i amesema wafungwa hao watafunguliwa mashtaka ya kutoroka gerezani bila idhini huku uchunguzi zaidi ukiendeleasa. Aidha, ameongeza kwamba jumla ya maafisa tisa wa magereza watashtakiwa kufuatia kutoroka kwa washukiwa hao.

Sita miongoni mwao akiwamo aliyekuwa Mkuu wa Gereza la Kamiti, Charles Mutembei leo wamefikishwa katika Mahakama ya Kahawa huku upande wa mashtaka ukilenga kuwazuilia kwa siku nyingine 30.

Kuhusu hali ya usalama nchini, Matiang'i na Mutyambai wamewashauri Wakenya kuripoti matukio yoyote yanayohatarisha usalama, hasa kufuatia mapigano yanayoendelea nchini Ehiopia vilevile mvutano wa kubuni serikali huko Sudan huku akisema tayari hatua kadhaa zimechukuliwa kudumisha usalama katika viwanja vya ndege na maeneo ya usafiri.

Share this: