×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ibrahim Rotich akana kumuua mwanariadha Agnes Tirop

Ibrahim Rotich akana kumuua mwanariadha Agnes Tirop

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya aliyekuwa mwanariadha Agnes Tirop, Ibrahim Rotich  amekana shtaka la muua mwanariadha huyo.

Rotich ameomewa mashtaka baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiakili katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi mjini Eldoret hapo jana kama ilivyoamuru mahakama mnamo tarehe 9 mwezi huu wa Novemba.

Alipofikishwa mahakamani, Msajili wa Mahakama Kuu ya Eldoret Diana Milimo alitoa agizo la mshukiwa kuendelea kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Railways na kufanyiwa uchunguzi wa akili siku ya Jumatatu kabla ya kufikishwa mahakamani tena leo.

Mshukiwa anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Tirop aliyepatikana nyumbani kwake kwenye eneo la Iten katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet mnamo tarehe 13 Oktoba akiwa na majeraha tumboni na kwenye shingo.

Mshukiwa wa mauaji yake Rotich alikuwa amejaribu kutoweka nchini alipokamatwa kwenye eneo la Changamwe na maafisa wa polisi.

Share this: