×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ann Kananu aapishwa kuwa Gavana wa Nairobi

Ann Kananu aapishwa kuwa Gavana wa Nairobi

Anne Kananu Mwenda ameapishwa kuwa gavana wa tatu wa Kaunti ya Nairobi. Kananu ameapishwa katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi katika halfa fupi ambayo imekuwa na mbwembwe za aina yake ikiwamo kuwasilishwa kwa gari lenye muundo wa zamani.

Katika hotuba yake, gavana huyo ameahidi kurejesha hadhi ya jiji huku akiwaahidi wakaazi wa kaunti hii kwamba watapokea huduma bora hata zaidi chini ya utawala wake.

Awali, Barabara ya City Hall way ilifungwa kwa muda ili kupisha shughuli ya kumwapisha Kananu ambaye amekuwa Kaimu Gavana tangu Januari tangu kuapishwa katika wadhfa wa Naibu Gavana huku juhudi zake za kuapishwa kuwa Gavana zikizuiwa na kesi mahakamani.

Wakenya wanasubiri kufahamu nani atakayeteuliwa kuwa Naibu Gavana wa Anne Kananu ikisalia miezi takriban miaka kabla ya uchaguzi mku kufanyika.

Gavana Kananu Mwenda alifahamika kwa umma mara ya kwanza baada ya mtangulizi wake Mike Sonko kumteuwa kuwa naibu wake tarehe 6 mwezi Januari mwaka 2020.

Kabla ya uteuzi huo, Kananu alikuwa afisa aliyesimamia Idara ya Kukabili Majanga katika serikali ya Kaunti ya Nairobi, wadhifa aliohudumu kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo. Kabla ya hapo, alikuwa msimamizi wa idara ya usalama, kitengo cha kukagua ubora wa bidhaa katika mamlaka ya Viwanja vya Ndege, KAA kwa kipindi cha miaka 13.

Awali, alikuwa msaidizi katika kampuni ya uwakili ya H. Mogambi and Co Advocates na kisha katika Chuo cha Kenya College of Communications technology.

Gavana huyo ni mjane wa marehemu Philip Njiru Muthathai ambaye alifariki dunia mwezi Januari 2019 kufuatia ajali ya barabarani. Na sasa katika historia ya Kenya amekuwa gavana wa kike wa nne baada ya Anne Waiguru wa Kirinyaga, Charity Ngilu wa Kitui na marehemu Joyce Laboso aliyeiongoza kaunti ya Bomet.

Awali, uteuzi wake ulikumbwa na utata baada ya Mahakama Kuu kuzuia kuchujwa kwake na Bunge la Kaunti ya Nairobi kufuatia kesi iliyowasilishwa na Mkenya peter Adhiambo Agoro ambaye alidai kwamba Sonko alikiuka sheria kwa kumteua Kananu kutwaa wadhifa ambao ulisalia wazi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Share this: