×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raila apeleka Azimio la Umoja Kilifi

Raila apeleka Azimio la Umoja Kilifi

Kiongozi wa ODM, Raila Odinga amepeleka kampeni za Azimio la Umoja katika Kaunti ya Kilifi.

Raila ameandamana na viongozi mbalimbali akiwamo Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui, wa Machakos Alfred Mutua miongoni mwa viongozi wengine huku akilakiwa na viongozi kadhaa wa Pwani wakiongozwa na Mbunge wa Ganze, Teddy Mwabire ambaye vilevile ndiye Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha ODM na Seneta Stewart Madzayo.

Magavana wa Kilifi, Amason Jeffa Kingi na mwenzake wa Mombasa Ali Hassan Joho hata hivyo hawajahudhuria huku Gavana Kinyanjui wa Nakuru akiwahakikishia wanaohudhuria kwamba Raila ataungwa mkono katika Mlima Kenya.

Katika Kaunti ya Meru, Naibu wa Rais William Ruto naye ameendelea kumshambulia Raila Odinga na kumhusisha na vurugu. Kadhalika amemrai Gavana Kiraitu Murungi kutowashinikiza wakazi kumuunga mkono Raila Odinga.

Share this: