×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Miguna Miguna kurejea nchini Jumanne 16

Miguna Miguna kurejea nchini Jumanne 16

Wakili mwenye Utata Miguna Miguna amesisitiza kwamba atarejea nchini Jumanne wiki ijayo.

Miguna ambaye kwa sasa yupo Brandenburg Gate, Berlin amesema anatarajiwa kuwasili nchini saa tatu asubuhi jinsi ilivyopangwa awali.

Kupitia mtandao wa twitter, Miguna ameendelea kupuuza hatua ya mahakama kutupilia mbali ombi la kutaka vizuizi kuondolewa.

Katika uamuzi wa jana, Jaji Hedwig Ongudi alisema ombi hilo halikuambatanishwa na ushahidi wa kuwapo maagizo hayo.

Hata hivyo, Miguna alisema hatambui uamuzi wa jana na kwamba atafuata ule uliotolewa na majaji Chacha Mwita Desemba 14, 2018 na Weldon Korir Januari 6, 2020. Kulingana na mawakili ni kwamba uamuzi wa jana unamaanisha vizingiti dhidi ya safari ya Miguna kurejea nchini vingalipo.

Aliyekuwa Jaji Mkuu Willy Mutunga ni miongoni mwa wanaharakti ambao wamejitolea kuandamana naye ili kuhakikisha kwamba maagizo ya mahakama yanaheshimiwa.

Miguna amefanya majaribio ya kurudi Kenya mara  mbili baada ya kufurushwa kwa kumwapisha Kinara wa ODM, Raila Odinga kuwa rais wa wananchi ila hajafanikiwa.

Share this: