×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto akita kambi Kiambu kutangaza ajenda zake

Ruto akita kambi Kiambu kutangaza ajenda zake

Naibu wa Rais William Ruto amerejea tena katika eneo la Kati leo hii ambapo amepeleka kampeni zake za kumuinua Mkenya wa kipato cha chini.

Ruto ambaye amefanya ziara katika maeneo  ya Ngoriba, Gatuanyaga, Makongeni na Kiganjo huku akiwashauri wakazi kumchagua kiongozi anayewafaa wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Ameendelea kumshtumu Kiongozi wa ODM Raila Odinga akisema mipango waliyokuwa nayo na Rais Uhuru Kenyatta wakati alipoanza kushirikiana na kiongozi huyo.

Naibu huyo wa rais alikuwa ameandamana na wabunge kadhaa akiwamo Adan Duale wa Garissa Mjini na Kimani Ichungwa wa Kikuyu, ambao wamemkosoa vikali Gavana wa Kitui Charity Ngilu kufuatia matamshi yake dhidi ya Ruto hapo jana wakati wa Ziara ya Raila Odinga katika eneo la Ukambani.

Ruto pia amefanya ziara katika Eneo Bunge la Gatundu Kaskazini. Hata hivyo hakuelekea Eneo Bunge la Gatundu Kusini anakotoka Rais Uhuru Kenyatta.

Hayo yanajiri huku Kiongozi wa ODM Raila Odinga akiwasili Kilifi tayari kwa ziara ya siku tatu katika eneo la Pwani. Raila amefanya mkutano na Kiongozi wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU Francis Atwoli.

Ataanza ziara yake kesho kwa akuhudhuria ibada katika eneo la Mpeketoni. Jumatatu ataelekea Malindi kwenye Kaunti ya  Kilifi kabla ya kukamilisha ziara hiyo Jumanne katika maeneo ya Kwale, Likoni na  Mombasa.

Share this: