×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mshukiwa wa ugaidi Abdulahhi Hussein akamatwa Lang'ata

Mshukiwa wa ugaidi Abdulahhi Hussein akamatwa Lang'ata

Maafisa wa Polisi wanaendelea kumzuilia mshukiwa wa ugaidi ambaye alikamatwa katika eneo la Lang'ata Nairobi.

Mshukiwa huyo alitambuliwa kuwa Abdulahhi Hussein raia wa Somalia.

Kulingana na taarifa ya DCI, mshukiwa huyo alifika kwa afisa mmoja wa polisi alipokuwa akishika doria mwendo wa saa nane usiku na kutaka taarifa muhimu kutoka kwake. Mshukiwa aliahidi kumpa afisa huyo shilingi elfu mia moja themanini ili kumpa taarifa hizo.

Hata hivyo afisa huyo alikataa na kuwajulisha wenzake ambao walifika walikokuwa na Alipatikana na dola za Marekani ambazo ni sawa na shilingi elfu mia moja hamsini na sita  zak Kenya.

Mkuu wa polisi wa Langata Benjamin Mwanzi amesema wanachunguza kubaini lengo la mshukiwa huyo lilikuwa lipi.

Haya yanajiri wakati ambapo taifa liko katika tahadhari ya usalama hasa kufuatia agizo la Rais hapo jana kwa vikosi vya usalama kuimarisha doria ndani na nje ya nchi.

Leo hii Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai amewaagiza maafisa wote walio likizoni kurejea kazini mara moja kuanzia Jumatatu.

Share this: