×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwendwa kusalia katika seli za polisi wikendi

Mwendwa kusalia katika seli za polisi wikendi

Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini FKF aliyebanduliwa Nick Mwendwa atalazimikika kusalia korokoroni wikendi nzima.

Mwendwa aliyekamatwa jana, anazuiliwa katika Kituo cha polisi cha Muthaiga. 

Wakili wake Eric Mutua, ameliambia gazeti la The Standard kuwa mteja wake ataendelea kuhojiwa na kuulizwa maswali  akisema anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu

Mwendwa anayechunguzwa kufuatia tuhuma mbalimbali za ufisasdi alikamatwa baada ya kukataa kuondoka ofisini licha ya Wizara ya Michezo kuivunja bodi ya FKF na kubuni kamati ya muda.

Wakati uo uo, Muungano wa Vyama vya wafanyakazi COTU umempongeza Waziri wa Michezo Amina Mohammed kwa kumbandua.

Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli amesema sekta ya soka nchini ilikuwa imedorora kutokana na uongozi mbaya wa Mwendwa.

Alhamisi wiki hii Waziri Amina aliivunja bodi ya FKF na kubuni kamati ya muda kuongoza shughuli za shirikisho hizo. 

Haya yanajiri huku Shirikisho la Soka Duniani likitishia kuipiga Kenya marufuku iwapo shughuli za mchezo huo nchini zitaendelea kuendeshwa na kamati hiyo ya muda.

Licha ya Fifa kutoa onyo, Waziri wa michezo Mohammed alichapsha majina na wanakamati wote ambao waliteuliwa kwenye gazeti rasmi la serikali. Kamati hiyo inayoongozwa na Jaji Mstaafu Aaron Ringera  ilitangaza kusitisha ligi zote tano nchini kwa wiki mbili.

Share this: