×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Koome kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kumshurutisha Rais kuwaidhinisha majaji 6

Koome kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kumshurutisha Rais kuwaidhinisha majaji 6

Jaji Mkuu Martha Koome, sasa amewasilisha notisi ya rufaa kupinga agizo la Mahakama ya Juu kumtaka kuwaapisha majaji sita walioachwa nje na Rais Uhuru Kenyatta.

Katika ombi ambalo limewasilishwa na Kampuni ya Uanasheria Muma&Kanjama Advocates, Koome amesikitishwa na agizo hilo akisema atakata rufaa.

Punde tu baada ya agizo hilo, Koome aliwasuta majaji wa Mahakama Kuu akisema tayari alikuwa katika majadiliano na Rais ili sita hao waidhinishwe.

Kwa mujibu wa Koome, agizo hilo lilizua mkanganyiko na kulemaza juhudi alizokuwa amepiga. Aidha, awali Koome alisisitiza kwamba ni sharti sita hao waidhinishwe ili kuungana na wenzao 34 walioadhinishwa.

Hata hivyo, Rais wa Chama cha Wanasheria, LSK Nelson Havi alimtaka Koome kudhihirisha uwezo wake kisheria.

Katika ujumbe, Havi alisema agizo la mahakama lilikuwa jaribio tu na lililenga kuweka wazi msimamo wa Jaji Koome.

Ikumbukwe tayari rufaa iliwasilishwa kwenye Mahakama ya Rufaa na uamuzi unasubiriwa. Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwasilisha ombi akitaka agizo hilo kusitishwa.

Mahakama Kuu ilitoa makataa ya siku kumi nne kwa Rais kuwaidhinisha sita hao, la sivyo waidhinishwe na Jaji Mkuu.

Miongoni mwa sita hao ni George Odunga, Joel Ngugi na Aggrey Muchelule.

Share this: