×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Boeing itawafidia waathiriwa wa ajali ya ndege ya Ethiopia

Boeing itawafidia waathiriwa wa ajali ya ndege ya Ethiopia

Hatimaye kampuni ya Boeng' imeafikiana na familia za watu mia moja hamsini na saba waliofariki kufuatia ajali ya ndege ya Ethiopia mwaka 2019. Kulingana na stakabadhi za mahakama moja katika jimbo la Chicago Marekani kampuni ya Boeng imekubali kuwajibika kufuatia ajali hiyo iliyohusisha moja ya ndege zake aina ya 737 Max.

Shirika la Habari la BBC limeripoti kwamba familia za walioaga dunia zimekubali kwamba hazitawasilisha ombi kutaka kampuni hiyo iadhibiwe.

Makubaliano hayo sasa yanatoa nafasi kwa familia kwenye mataifa mengine kama vile Kenya na Ethiopia kuomba fidia kupitia mahakama za Marekani badala ya zile za mataifa yao hatua inayoweza kuaithiri mpango wa kufidiwa au hata kusababisha kupungua kwa fidia yenyewe.

Wakenya thelathini na wawili walifariki dunia kufuatia ajali hiyo.

Mawakili Robert Clifford, Steven Marks na Justin Green walioziwakilisha familia za waliofariki katika kesi hiyo wamefurahishwa na hatua zilizoafikiwa wakisema haki itapatikana.

Share this: