×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watoto wachanga zaidi ya milioni 22 walikosa chanjo ya ukambi mwaka, 2020

Watoto wachanga zaidi ya milioni 22 walikosa chanjo ya ukambi mwaka, 2020

Zaidi ya watoto wachanga milioni ishirini na mbili kote duniani hawakuchanjwa dhidi ya ugonjwa wa Ukambi yaani Measles mwaka 2020. Kulingana na utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani WHO kwa ushirikiano na Kituo cha Kudhibiti Maambukizi ya Magonjwa cha Marekani CDC,  idadi hii ni milioni tatu zaidi ya waliokosa kuchangwa mwaka 2019.

Ripoti hiyo aidha inaonesha kwamba idadi ya watu walioripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo ilipungua kote duniani mwaka jana kwa asilimia 80 kulinganishwa na mwaka 2019.Hata hivyo huenda hali hiyo ilitokana na kupungua kwa kampeni za ukaguzi, upimaji na kuripotiwa kwa ugonjwa huo kutokana na janga la korona.

Mkurugenzi wa CDC Marekani anayesimamia kitengo cha utoaji chanjo duniani Kevin Cain amesema huenda hali hii ikayarejesha nyuma mataifa mengi yaliyokuwa yamepiga hatua ya kuangamiza ugonjwa huo.

Cain amesema kampeni ishirini na nne zilizokuwa zimepangwa katika mataifa ishirini na matatu za utoaji chanjo dhidi ya ukambi ziliahirishwa kutokana na korona, hali ambayo inawaweka hatarini zaidi ya watu milioni tisini na watatu.

Mkurugenzi wa utoaji chanjo katika WHO Daktari Kate O’Brien, amesema kuna haja ya mataifa kuweka mikakati ya dharura haraka iwezekanavyo ili kuzuia mlipuko wa ukambi na vifo katika siku zijazo.

Kulingana na WHO ukambi ni miongoni mwa magonjwa yanayoambukizwa kwa urahisi na haraka lakini unaweza kuzuiwa kufuatia chanjo. Katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita chanjo dhidi ya ukambi imezuia vifo vya zaidi ya watu milioni thelathini kote duniani. Takwimu za WHO zinaonesha kwamba maambukizi ya ukambi yamepungua kutoka zaidi ya milioni moja mwaka 2000 hadi elfu sitini mwaka 2020.

Share this: