×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwanamke akamatwa Kasarani kwa kumtilia ''mchele'' mwanamme mmoja

Mwanamke akamatwa Kasarani kwa kumtilia ''mchele'' mwanamme mmoja

Makachero wa Idara ya Upelelezi, DCI wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 30 kwa madai ya kumtilia mwanaume mmoja vidonge vya kumfanya kupoteza fahamu, kwa jina la mtaani mchele, kisha kumwibia shilingi milioni moja.

Mkurugenzi wa DCI, George Kinoti amesema mwathiriwa na rafikiye wa kiume walikuwa katika klabu moja mtaani Embakasi walipokutana na mwanamke kwa jina Virginia Wangui Thiga pamoja na rafikiye.

Wawili hao, walimkaribisha Virginia na rafikiye kwa vinywaji kabla ya tukio hilo kufanyika.

Mwendo wa saa kumi alfajiri leo hii, wanne hao walielekea katika chumba cha kukodi. Hata hivyo, dakika chache baadaye, rafikiye mwathiriwa aliondoka huku akimwacha na wanawake hao wawili.

Mwanamme huyo amewaambia polisi kwamba wanawake hao walimwibia simu, kadi ya ATM na kitambulisho chake.

Aligundua baadaye kwamba shilingi milioni moja zilikuwa zimeibwa kutoka akaunti yake ya benki.

Virginia ambaye amenaswa mtaani Kasarani, anazuiliwa na polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Mshukiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Share this: