×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ibrahim Rotich, mshukiwa mkuu wa mauaji ya Agnes Tirop kufanyiwa uchunguzi wa akili

Ibrahim Rotich, mshukiwa mkuu wa mauaji ya Agnes Tirop kufanyiwa uchunguzi wa akili

Mahakama Kuu ya Eldoret imeagiza Ibrahim Rotich, mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanariadha Agnes Tirop kufanyiwa uchunguzi wa akili katika Hospitali ya Rufaa ya Moi kabla ya kufunguliwa na mashtaka.

Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Diana Milimo aidha amewataka maafisa wa wanaochunguza mauaji hayo kumwasilisha Rotich aliyekuwa mpenzi wa Tirop mahakamani Novemba 16 ili akabiliwe na mashtaka ya mauaji ya mwanariadha huyo.

Wakili wa upande wa mashtaka, David Fedha ametoa ombi hilo kwa mahakama, ombi ambalo awali wakili anayemwakilisha Rotich, Ngige Mbugua alikuwa ameliwasilisha katika Mahakama ya Iten.

Katika kesi hiyo inayolenga kubaini aliyetekeleza mauaji ya mwanariadha huyo aliyeiletea sifa Kenya kwenye mashindano ya kimataifa, mshukiwa Rotich mara ya kwanza aliwasilishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Iten, Naomi Wairimu baada ya kuzuiliwa kwa siku 20 ili kupisha uchunguzi.

Hakimu Wairimu aliagiza mshukiwa huyo kuwasilishwa mbele ya Mahakama Kuu ya Eldoret leo ambapo sasa atashtakiwa Jumanne wiki ijayo kwa tuhuma za mauaji.

Tirop alipatikana amefariki dunia Oktoba 13, nyumbani kwake mjini Iten alikokuwa akiishi na Rotich. Ripoti ya upasuaji aidha inaonesha kwamba aliaga dunia kwa kupigwa shingoni vilevile kiunoni.

Share this: