×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KEPSA yashirikiana na ABSA kuboresha mfumo wa ajira kwa vijana

KEPSA yashirikiana na ABSA kuboresha mfumo wa ajira kwa vijana

Huku serikali ikijizatiti kuboresha mfumo wa utoaji ajira kwa vijana kidijitali, Muungano wa Mashirika ya Sekta ya Binafsi, KEPSA na Benki ya ABSA zimezindua mpango wa kuwawezesha mamilioni ya vijana wanaotafuta nafasi za kazi mitandaoni kupitia mipango yao ya - Ajira Digital na Ready-to-Work.

ABSA inalenga kuwafanyia mafunzo vijana kupitia Ready-to-Work ili kuhakikisha wanapata ujuzi wa kujitosa kikamilifu katika sekta hiyo inayoendelea kukua.

Mpango huo unalenga kupiga jeki ule wa serikali wa kubuni nafasi za kazi, hivyo kusuluhisha changamoto za ukosefu wa ajira nchini.

Afisa Mkuu Mtendaji wa KEPSA, Carole Kariuki amesikitikia idadi kubwa ya vijana wasiokuwa na ajira, akisema mikakati inapaswa kuwekwa ili kuhakikisha upatikanaji wa ajira kufikia mwaka wa 2030.

Meneja Mkuu wa ABSA, Jeremy Awori kwa upande wake amesema benki hiyo inashirikiana na sekta zote ili kuboresha mazingira ya kufanyia kazi nchini. 

Share this: