×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Linturi ataka arejeshewe laki mbili zilizopewa mlalamishi aliyedai alitaka kumbaka

Linturi ataka arejeshewe laki mbili zilizopewa mlalamishi aliyedai alitaka kumbaka

Seneta wa Meru Mithika Linturi sasa anaitaka mahakama kumrejeshea shilingi laki mbili zilizokabidhiwa mwanamke mmoja anayedaiwa kujaribu kumbaka.

Linturi anatuhumiwa kuingia kwa siri katika hoteli mmoja mjini Nanyuki na kujaribu kumbaka .

Kupitia wakili wake Muthomi Thiankolu, Linturi amemwambia Hakimu wa Mahakama ya Milimani Susan Shitubi kwamba anahitaji fedha hizo ambazo upande wa mashtaka ulimpa mlalamishi mwaka uliopita.

Wakili huyo ameitaka mahakama kuagiza serikali kumpa taarifa za mashahidi na ya polisi kuhusu kesi hiyo.

Wakili wa upande wa mashtaka Alice Mathangani ameimbia mahakama kwamba afisi wa uchunguzi anataka muda zaidi kupitia stakabadhi hizo kabla ya kuupa upande wa mshtakiwa.

Aidha amesema fedha anazotaka Linturi ni ushahidi kuwa alilenga kuzima kesi hiyo kwa kumpa mwanamke huyo shilingi laki mbili hivyo basi atapewa tu baada ya kesi kukamilika.

Januari tarehe 30 mwaka huu mwenda wa saa tisa alfajiri usiku katika Hoteli ya Maiyan , Linturi anadaiwa kuingia katika chumba alikokuwa amelala mwanamke huyo kabla ya kuanza kumpapasa.

Mmwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 anadai kwa alikua ameuacha mlango wazi baada ya kuafikiana na mmumewe ambaye baadaye angejiunga naye chumbani.

Anadai aligundua baada ya dakika thelathini kwamba jamaa aliyekuwa kitandani hakuwa mumewa bali Linturi kabla ya kupiga mayowe.Ili kuzuia kisa hicho kujulikana alimpa fedha hizo shilingi laki mbili na ahadi za kumpa nyingine kabla ya kukosa kufanya hivyo. Kesi hiyo itatajwa baada ya wili mbili.

Share this: