×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Smokin Wanjala, Mohammed Ibrahim na Njoki Ndung'u hawatajiondoa katika kesi ya BBI

Smokin Wanjala, Mohammed Ibrahim na Njoki Ndung'u hawatajiondoa katika kesi ya BBI

Rufaa iliyowasilishwa kupinga uamuzi wa kuharamisha ripoti ya Mpango wa BBI, itasikilizwa kuanzia tarehe 18 hadi 20 mwezi Januari, 2022.

Katika mwongozo ambao umetolewa leo hii, Jaji Mkuu Martha Koome amesema mahakama itachukua siku tatu kisha kutenga siku ya uamuzi. .

Katika vikao vya leo asubuhi, mahakama imepuuza ombi la Wakili Isaac Aluochier kutaka majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala na Njoki Ndung'u kuondolewa katika jopo linalosikiliza rufaa hiyo akiwashtumu kwa kukosa maadili.

Kwa mujibu wa Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu, mlalamishi ambaye hakuwasilisha ushahidi wa kutosha dhidi ya watatu hao hivyo watasalia kwenye jopo hilo la majaji sita. Aidha, Mwilu amesema Tume ya Huduma za Mahakama, JSC haijapokea malalamiko kuhusu majaji hao.

Pia mahakama imetupilia mbali ombi la chama cha PNU kutaka kujumuishwa katika kesi hiyo.

Jaji Mkuu Martha Koome anaongoza vikao vya leo ambapo wametoa uamuzi mbalimbali kuhusu rufaa

Koome anaongoza majaji  hao kutaja na kutoa mwelekeo wa rufaa zilizowasilishwa kupinga kutupiliwa mbali kwa kesi ya BBI.  Koome amesema kutokana na janga la korona, amelazimika kuwapunguza mawakili hadi mmoja kila upande, huku wengine wakifuatilia mitandaoni.

Koome amekubali ombi la mawakili kuongeza siku za kuwasilisha stakabadhi mahakamani hadi 15 badala ya tano.

Hata hivyo, amekubali Ombi la Martha Karua kuwasilisha utetezi wao kwa maandishi hadi kurasa 30, huku akikata ombi la Havi kutaka kurasa hizo kuwa 40 badala ya 15.

Share this: