×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wanafunzi kadhaa kukesha korokoroni baada ya kukamatwa

Wanafunzi kadhaa kukesha korokoroni baada ya kukamatwa

Wanafunzi kumi na mmoja wa shule za upili za Kagumo na Kiandu watasalia korokoroni hadi Jumatano watakapofunguliwa mashtaka ya kujaribu kuteketeza shule zao.

Wanafunzi hao wamefikishwa katika Mahakama ya Nyeri ila hawakuruhusiwa kukiri au kukana mashtaka dhidi yao.

Wanafunzi watatu wa Shule ya Upili ya Kagumo wanatuhumiwa kushirikiana  kuteketeza sehemu ya shule yao Jumapili usiku.

Aidha, wenzao wanane wa Kiandu watashtakiwa kwa kukataa kuwafichua walioteketeza shule yao.

Mahakama imeagiza Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma, ODPP kuwasilisha stakabadhi za washukiwa, na kuwatumia baadhi yao kuwa mashahidi.

Wanafunzi hao watasalia katika vituo vya polisi vya Kiganjo na Nyeri wakisubiri kurejeshwa mahakamani.

Haya yanajiri huku wanafunzi wengine sita wa Shule ya Wavulana ya Maranda wakikesha korokoroni hadi kesho watakapofikishwa mahakamani.

Mkurugenzi wa Elimu katika Kaunti ya Siaya, Nelson Sifuna amesema sita hao wamekamatwa baada ya kamera za CCTV kuonesha wakitoka katika bweni, muda mfupi baada ya mkasa wa moto.

Wanahusishwa na kisa cha kuteketeza bweni katika shule hiyo usiku wa kuamkia leo.

Aidha, shule hiyo imefungwa kwa muda usiojulikana ili kuruhusu uchunguzi kufanywa.

Wakati uo huo, Mshirikishi wa Utawala katika eneo la Nyanza, Magu Mutindika amebuni jopo maalumu kuchunguza kiini cha visa vya mioto shuleni

Share this: