×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakili Nandwa apatikana akiwa hai uko Mwingi

Wakili Nandwa apatikana akiwa hai uko Mwingi

Wakili Profesa Hassan Nandwa, aliyetekwa nyara siku kumi na moja zilizopita amepatikana akiwa hai katika eneo la Mwingi, Kaunti ya Kitui. Inaarifiwa kuwa Nandwa aliachiliwa saa saba usiku wa kuamkia leo na tayari amekutana na familia yake.

Alitekwa nyara tarehe 29 Oktoba, baada ya kuachiliwa kwa mteja wake Elgiva Bwire, mshukiwa mkuu wa ugaidi.

Bwire vilevile alitekwa nyara na bado hajapatikana. Hata hivyo haijabainika ni nani aliwateka nyara. Nandwa anaendelea na matibabu, huku Chama cha Wanasheria, LSK kikishinikiza kuachiliwa kwa mteja wake.

LSK imeonya kwamba iwapo Bwire hataachiliwa baada ya siku 30, watalazimika kuwasilisha kesi mahakamani kuishtaki serikali.

Wakati uo huo, viongozi wa dini ya Kiislamu wamekashifu visa vya utekaji nyara, na kuitaka serikali kuwakabili wahusika.

Share this: