×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Polisi apigwa Kariokor Nairobi

Polisi apigwa Kariokor Nairobi

Afisa wa Polisi wa Trafiki anauguza majeraha mabaya usoni baada ya kushambuliwa na mtu mmoja jana jioni hapa jijini Nairobi.

Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi, DCI George Kinoti amesema afisa huyo alikuwa kazini kwenye mzunguko wa Kariokor, wakati mwanamme mmoja alifika na kumpiga usoni kisha kumkata kwa kifaa butu, hali iliyomsababishia majeraha mabaya.

Ilimlazimu mhudumu wa bodaboda kumsaidia kwa kumpeleka hospitalini ambapo alitibiwa jana usiku na kuruhusiwa kuondoka.

Tukio hilo lilisababisha msongamano mkubwa wa magari kwani hapakuwapo na polisi aliyekuwa akiyadhibiti magari.

Kinoti sasa amewaomba wananchi kushirikiana nao katika kuwatambua wahalifu wanaowashambulia polisi na hata umma ili hatua zichukuliwe.

Share this: