×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakuu wa KEMSA washtakiwe-Kanini Kega

Wakuu wa KEMSA washtakiwe-Kanini Kega

Mjadala kuhusu hali katika Mamlaka ya Usambazaji Dawa KEMSA, ungali unaendelea nchini, huku viongozi mbalimbali wakiendelea kushinikiza kushtakiwa kwa wakuu wa mamlaka hiyo waliohusishwa na sakata mbalimbali za ufisadi.

Mbunge wa Mwingi Magharibi, Charles Nguna na Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Machakos, Joyce Kamene wamemrai Rais Uhuru Kenyatta kutobuni tena jopo maalumu la kuchunguza wizi huo.

Akihutubu kwenye eneo la Sikhendu katika Kaunti ya Trans Nzoia, Mbunge wa Bobasi, Innocent Obiri amesema ni ukiukaji wa Katiba kuwalenga maafisa wasio na jukumu kubwa kwenye KEMSA na kuwaacha maafisa wakuu.

Ni usemi ambao umesisitizwa na Mbunge wa Kiminini, Daktari Chris Wamalwa.
Kauli za viongozi hawa zinajiri wakati ambapo Shirika la Kitaifa la Huduma za Vijana NYS likikana taarifa kwamba limetwaa usimamizi wa KEMSA.

Wiki hii Waziri wa Afya mutahi Kagwe anatarajiwa kufike mbele ya Seneti ili kutoa mwanga zaidi kuhusu usimamizi wa Mamlaka hiyo. Wiki jana zaidi yawafanyakazi mia tisa waliagizwa kufanyia kazi nyumbani kwa kipindi cha wiki moja ili kupisha tathimini. Hata hivyo,  baadhi wamehofia kwamba huenda hatua hiyo ikawa mwanzo wa kuwaachisha kazi.

Share this: