×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kalonzo amkaribisha Ruto Ukambani

Kalonzo amkaribisha Ruto Ukambani

Kiongozi wa Wiper Kalonzo amemkaribisha Naibu wa Rais William Ruto kuzuru eneo la Ukambani akisema kila mwanasiasa ana haki ya kuzuru eneo lolote nchini kupigia debe ajenda yake.

Kalonzo hata hivyo, amemtaka Ruto aweke wazi namna alivyopata mali zake na fedha ambazo ameendelea kuwapa Wakenya. Ametilia shaka namna Ruto amepata utajiri wake kwani mshahara wake hauwezi kumwezesha kutumia fedha jinsi anavyofanya.

Kalonzo aidha amewataka Wakenya kutowachagua viongozi ambao maadili yao yanatiliwa shaka wakati wa uchaguzi wa mwaka ujao.

Akizungumza katika eneo la Mwingi Magharibi wakati wa hafla mbalimbali, Kalonzo amesema baadhi ya viongozi wameendelea kupora mali ya umma kwenye mashirika mbalimbali yakiserikali mfano Kenya Power na kusababisha gharama ya kawi kupanda.

Kiongozi huyo amesema wakati umefika kwa Wakenya kuwakataa viongozi wanaotumia fedha za wizi kuwahonga.

Share this: