×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raila kutangaza azma ya kuwania urais Desemba 9 2021

Raila kutangaza azma ya kuwania urais Desemba 9 2021

Huku kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka ujao zikiendelea kushika kasi, Kiongozi wa ODM Raila Odinga, atatangaza rasmi azma yake ya kuwania urais mwaka ujao tarehe 9 Mwezi Desemba

Akihutubu wakati wa misururu ya mikutano hapa jijini Nairobi, Odinga aidha amesema atawashirikisha wafuasi wake kabla kutoa tangazo hilo.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, iwapo atatwaa nafasi ya urais, bei ya bidhaa za kimsingi itashuka. Pia amewahimiza vijana kujiandikisha kuwa wapigakura katika ofisi za Tume ya Uchaguzi, IEBC.

Vilevile, Odinga amekariri kwamba ODM na Jubilee zitabuni muungano hivi karibuni na utakuwa imara zaidi. Amewataka washindani wake kujiandaa kwa kivumbi kikali.

Odinga ametumia fursa hiyo kuwasuta Naibu wa Rais William Ruto na wandani wake kwa kukejeli mpango wake wa kutoa shilingi elfu sita kwa familia iliyo na mtu asiye na kazi. Amesema pendekezo hilo linawezekana iwapo mianya ya ufisadi itazibwa.

Wakati uo huo, aliyekuwa Mbunge wa Gatanga Peter Kenneth ambaye anapigiwa upatu kuwa mgombea mwenza wa Odinga, amemhakikishia kwamba eneo zima la Mlima Kenya litamuunga mkono. Kenneth amemtaja Odinga kuwa kiongozi mwenye maadili hivyo haja ya kuongoza taifa hili. Amekashifu siasa za Wilbaro.

Viongozi wengine walioandamana na Odinga ni Mbunge wa Mathare, George Aladwa na Junet Mohammed wa Suna Mashariki. Viongozi hao wamehudhuria ibada katika Kanisa la Legio Maria-Makongeni kabla kufanya ziara jijini.

Share this: