×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Niko tayari kushirikiana na viongozi wengine-Ruto

Niko tayari kushirikiana na viongozi wengine-Ruto

Naibu wa Rais William Ruto amesema yu tayari kushirikiana na viongozi wengine ambao si wanachama wa UDA ili kubuni serikali baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Ruto ameashiria kumlenga Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, ambaye hivi majuzi alisema kwamba yu tayari kufanya kazi naye.

Akizungumza alipohudhuria ibada katika Kanisa la AIPCA Kikopey Gigilgil Nakuru , Ruto ameshikilia kwamba chama cha UDA ndicho kitakachobuni serikali inayajo.

Kauli ya Ruto ilisisitizwa na wandani wake, akiwamo Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, Rigathi Gachagwa wa Mathira na Seneta wa Nakuru Susan Kihika. Viongozi hao wamepuuza juhudi za Raila kutafuta uungwaji mkono katika eneo la Mlima kenya wakisema Ruto ndiye maarufu.

Baadaye Ruto alihutubia umma katika maeneo ayo hayo ya Kikopey, Gilgil na Naivasha ambapo aliendelea kupigia debe mpango wake wa kumuinuia Mkenya wa Kipato cha chini iwapo atachaguliwa kuwa rais mwaka ujao.

Amerejelea kwamba ataendeleza agenda za Rais Uhuru Kenyatta.

Share this: