×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

IMF yakubali kuipa Kenya Ksh29.4B

IMF yakubali kuipa Kenya Ksh29.4B

Shirika la Fedha Duniani, IMF limekubali kuipa Kenya shilingi bilioni 29.4 zaidi ili kuisadia kuongeza mgao wa fedha katika bajeti ya kushughulikia masuala mbalimbali likiwamo janga la korona.

Hatua hii inafuatia maafikiano baina ya maafisa wa IMF na serikali ya Kenya kuhusu vigezo vya mpango wa shilingi bilioni 256  zinazolengwa kutolewa kwa Kenya kuimarisha hali yake ya kifedha.

Iwapo Bodi simamizi ya IMF itaidhinisha makubaliano hayo basi inamaanisha Kenya itakuwa imepokea shilingi bilioni 109.7 kutoka kwa shirika hilo katika mwaka wa kifedha wa 2020/2021

Kulingana na IMF mapato yanayotokana na kodi yameongezeka, hali itakayoisadia hazina ya kitaifa kukoma kutegemea mikopo kufanikisha bajeti ya nchi.

Miongoni mwa maafikiano ni kwamba baadhi ya taasisi za serikali zitafanyiwa mabadiliko hali ambayo huenda ikasababisha wafanyakazi wengi kupoteza nafasi zao za kazi. Baadhi ya taasisi aidha zitaunganishwa na nyingine kubinafsishwa.

Taasisi ambazo tayari zimeanza kuathirika na mpango baina ya Kenya na IMF ni Kampuni ya Usambazaji Umeme Kenya Power na Shirika la Ndege la Kenya Airways.

Wakati uo huo IMF imesema licha ya uchumi wa nchi kuanza kuimarika baada ya kuathiriwa na janga la korina, ukame katika eneo la Kaskazini Mashariki na utovu wa usalama katika baadhi ya maeneo unaweza kulirejesha tena nyuma taifa hili.

Share this: