×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mbunge atishia kuelekea mahakamani kupinga jesho kusimamia KEMSA

Mbunge atishia kuelekea mahakamani kupinga jesho kusimamia KEMSA

Mzozo wa Usimamizi wa Mamlaka ya Usambazaji Dawa KEMSA huenda ukaishia mahakamani baada ya viongozi kadhaa kutishia kuwasilisha kesi mahakamani.

Mbunge wa Kandara, Alice Wahome amesema atawasilisha kesi mahakamani kupinga hatua ya Idara ya Jeshi kusimamia Mamlaka ya Usambazaji Dawa KEMSA na mpango wa kuwafuta kazi zaidi ya wafanyakazi mia 900.  Seneta wa Narok Ledama ole Kina pia alitishia kuwasilisha kesi mahakamani kwa niaba ya wafanyakazi ambao huenda wakapoteza kazi.

Wahome  amesema hatua ya kuwaagiza wafanyakazi hao kufanyia kazi nyumbani ni mbinu tu ya kuwafuta kazi ilhali si wao waliohusika na sakata mbalimbali za ufisadi ambazo zimeikumba mamlaka hiyo.

Mbunge huyo amesema majukumu ya jeshi yamewekwa wazi katika katiba na anachofanya rais kuikabidhi idara hiyo mamlaka ya kusimamia taasisi za umma ni kinyume na sheria.

Amesema mkondo anaochukua Rais Uhuru Kenyatta haufai kwani unaweza kulemaza taasisi za umma kwani itakuwa vigumu kuwawajibisha kupitia Idara za Uchunguzi.

Wafanyakazi wa KEMSA zaidi ya mia tisa walianza kufanyia kazi nyumbani huku bodi ya mamlaka hiyo ikisema mpango huo ni wa mwezi mmoja tu ili kupisha tathimini ya utendakazi.

Ikumbukwe mbunge huyo aliwahi kushinda kesi dhidi ya Rais kufuatia mpango wake wa kutaka kumjumuisha katika Baraza la Mawaziri, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Jiji la Nairobi NMS Generali Mohammed Mbadi.

Tayari Maseneta wamemwagiza Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kufika mbele yake kuhojiwa kuhusu kunachoendelea katika KEMSA.

Share this: