×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

DPP apewa uwezo wa kuwashtaki Chris Okemo na Samwel Gicheru

DPP apewa uwezo wa kuwashtaki Chris Okemo na Samwel Gicheru

Mahakama ya Juu imeipa idhini Ofisi ya Mkuu wa Mashtaka kuendeleza juhudi za kuhakikisha  aliyekuwa Waziri wa Fedha Chris Okemo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Kenya Power, Samuel Gichuru wanafunguliwa mashtaka ya utakatishaji wa fedha katika Kisiwa cha Jersey nchini Uingereza.

Uamuzi huo umetolewa kufuatia mvutano wa muda mrefu kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na Ofisi ya Mkuu wa Mashtaka kuhusu nani aliye na mamlaka ya kufanikisha mikakati ya kuwaruhusu wawili hao kufunguliwa mashtaka Uingereza.

Mwaka 2018 Mahakama ya Rufaa ilitoa uamuzi ikiridhia ombi la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kwamba Mkuu wa Mashtaka hafai kuingilia masuala yanayohusu mataifa mengine baada ya serikali ya kisiwa cha New Jersey kuomba wawili hao wafunguliwe mashtaka kisiwani humo.

Hata hivyo, suala hilo lilielekezwa katika Mahakama ya Rufaa huku sasa Mkuu wa Mashtaka Noordin Haji akipewa uhuru wa kukwamua mikakati hiyo iliyokwama miaka 10 iliyopita.

Okemo na Gichuru wanatuhumiwa kufuja fedha za serikali kati ya mwaka 1998 na mwaka 2002 na kuzificha katika akaunti kisiwani New Jersey nchini Uingereza.

Ikumbukwe Kenya ina mkataba na kisiwa cha New Jersey kurejesha fedha za ufisadi zilizowekezwa katika aia hilo japo lazima wahusika wawajibishwe kwanza kisheria.

Share this: