×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakulima wa miwa wa Busia walalamikia kuhangaishwa na mwekezaji

Wakulima wa miwa wa Busia walalamikia kuhangaishwa na mwekezaji

Wakulima wa miwa katika Kaunti ya Busia wameendelea kulalamikia madai ya kuhangaishwa na mwekezaji mmoja wa kampuni ya kusaga sukari.

Licha ya kuwasilisha malalamishi yao kwa kiwanda hicho hakuna hatua ambayo imechukuliwa hadi sasa huku viongozi wa Busia wakifumbia macho matakwa yao.

Miongoni mwa malalamishi yao ni kucheleweshwa kwa malipo yao, kutokatwa kwa miwa kwa wakati, kutishiwa maisha, malipo duni na mwekezaji huyo kushirikiana na matapeli kuwakandamiza

Mwekezaji huyo aidha anadaiwa kuwaagiza baadhi ya wakulima kuondoa saini zao za kupinga ukandamizaji dhidi ya kampuni yake. Mmoja wa Wakulima hao Salim Wekoba ameeleza namna waliovyoitwa ofisini humo na kushurutishwa kufanya hivyo.

Haya yanajiri huku malalamiko yao yaliowasilishwa kupitia Naibu Mwenyekiti wa Shirika la Kutetea Maslahi ya Wakulima wa Miwa, WEDIA Joseph Barasa yakidhibitishwa na Mamlaka ya Kilimo na Chakula nchini, AFA.

Mwakilishi wa AFA Ukanda wa Magharibi Joseph Ochola amesema uchunguzi wao umebainisha kuwapo kwa madai ya hongo, miwa kuchelewa kukatwa na mwekezaji huyo kununua miwa kutoka kwa matapeli .

Mapema mwaka huu, Waziri wa Kilimo Peter Munya aliagiza AFA kuhakikisha kuwa kampuni za miwa zinatia saini mikataba mipya na wakulima kuhusu malipo yao.

Munya aligiza kampuni hizo kuwajibishwa iwapo zitachelewa kuwalipa walimu kwa wakati ama kuwakandamiza.

Share this: