×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mtu mmoja akufa moja Kakamega

Mtu mmoja akufa moja Kakamega
Mtu mmoja amefariki papo hapo huku juhudi za kumtafuta mwenzake aliyeanguka ndani ya Mto Nzoia Kaunti ya Kakamega zikiendelea baada ya wawili hao kugongwa na gari  katika barabara ya Mumias kuelekea Bungoma wakiwa kando ya daraja la mto huo.
 
Kulingana na walioshuhudia ni kwamba wawili hao waligongwa na gari kando ya daraja hilo na gari la kibinafsi lililokuwa likiendeshwa kwa kasi.
 
Kwa upande wake Mbunge wa Mumias Mashariki, Benjamin Washiali aliyefika mahala pa tukio ameiitaka serikali kuwachunguza madereva wa magari wanaosemekana kuendesha magari wakiwa walevi.
 
Ajali hiyo imethibitishwa na Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Mumias, Steven Muoni akisema mwili umepelekwa katika Hifadhi ya St. Marys Mumias.

Share this: