×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Dpp aendelea kupuuza juhudi za kumwondoa ofisini

Dpp aendelea kupuuza juhudi za kumwondoa ofisini

Kwa mara nyingine Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma DPP Noordin Haji amepuuzilia mbali juhudi za kutaka kumng'atua ofisini, akisema wanaofanya hivyo wanamwandama kutokana na hatua ambazo amechukua kufuatia kesi mbalimbali.

Ikumbukwe makundi mawili yaliwasilisha ombi katika Tume ya Huduma za Umma PSC yakitaka Haji kuondolewa katika wadhifa wake kwa madai ya kuhujumu uchunguzi wa kesi mbalimbali. Hata hivyo Haji alipinga maombi hayo mahakamani na uamuzi ukatolewa kusitisha mipango yote ya kumwondoa ofisini hadi kesi aliyowasilisha itakaposikilizwa na kuamulia.

Wakati uo huo, amekana madai ya kuwapo kwa tofauti baina yake na Idara ya Upelelezi DCI.

Akihojiwa katika Spice FM Haji amesema tatizo alilo nalo na Idara ya DCI ni kuharakisha uchunguzi na kusababisha kesi kupelekwa mahakamani bila ushahidi wa kutosha.

Share this: