×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mgogoro mwingine wanukia kuhusu ugavi wa fedha za kaunti

Mgogoro mwingine wanukia kuhusu ugavi wa fedha za kaunti

Mvutano baina ya magavana na Tume ya Ugavi wa Mapato CRA kuhusu kiwango cha fedha kinachopaswa kutengewa serikali za kaunti huenda ukaibuka tena, baada ya CRA kupendekeza kaunti zisambaziwe shilingi bilioni 370 mwaka ujao wa kifedha. Pendekezo hili ni kinyume na lile la magavana lililotolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Magavana lililoitaka CRA kuongeza mgao wa fedha kwa kaunti kwa takribani shilingi bilioni 11 ambapo kaunti zingepata jumla ya shilingi bilioni 381.

Tume hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wake Jane Kiringai aidha imependekeza shilingi trilioni 1.76 zitengewe erikali ya kitaifa , shilingi bilioni 6.8 zitengee Hazina ya Equalisation Fund, fedha  ambazo zinakadiriwa kupatikana kupitia ushuru wa hadi trilioni 2.14.

Wakati wa kikao na wanahabari, kiringai ametetea mapendekezo ya CRA, akieleza kwamba hatua hiyo imetokana na hali ngumu ya uchumi, hitaji la kulipa mikopo ya serikali, vilevile uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Kwa mujibu wa Kiringai, iwapo CRA ingetekeleza pendekezo la magavana, serikali ingelazimika kukopa fedha na kufadhili bajeti hiyo, hali ambayo ingezidi kumkandamiza mwananchi.

Chini ya uongozi wa Gavana wa Embu Martin Wambora, Baraza la Magavana limekuwa likilalamikia ukosefu wa fedha za kutosha kufanikisha miradi mbalimbali ya serikali huku mara si moja akikiri kwamba serikali za kaunt zinalazimika kukopa fedha ili kuendesha shughuli mbalimbali.

Share this: