×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wizar ya Elimu yatangaza likizo fupi kufuatia kukithiri kwa uteketezaji wa majengo ya shule

Wizar ya Elimu yatangaza likizo fupi kufuatia kukithiri kwa uteketezaji wa majengo ya shule

  Wizara ya Elimu imelazimika kutangaza likizo fupi(halfterm) kuanzia Novemba 19 hadi Novemba 23 katika shule za upili baada ya kukithiri kwa visa vya uteketezaji wa majengo ya shule. Kalenda ya masomo iliyochapishwa hapo awali na Wizara ya Elimu ilionesha kwamba hakungekuwa na mapumziko muhula wa pili na wanafunzi wangefululiza hadi Disemba 24.

Katika taarifa ya Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha, wakurugenzi wote wa elimu kwenye kaunti 47 nchini wameagizwa kuhakikisha shule hizo za upili zinakuwa na likizo hiyo kuanzia Novemba 19 hadi Novemba 23. 

Ikumbukwe shule zilifungwa kwa takriban wiki moja pekee muhula wa kwanza na kufunguliwa Oktoba 12 kwa muhula wa pili. Ratiba ya Wizara ya Elimu ya hapo awali haikuonesha ni lini wanafunzi wangepumzika muhula wa pili kwani ilionesha tu kwamba wangekuwa shuleni hadi Disemba 24 kisha kuchukua mapumziko ya wiki moja  kwa ajili ya Krismasi na mwaka mpya na kurejea Januari mbili. Usisahau pia michezo ilipigwa marufuku shuleni kutokana na janga la korona kumaanisha ni masomo tu shuleni.

Taarifa ya wizara imejiri wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la visa vya uteketezaji wa majengo ya shule ambapo kufukia sasa visa takirban 25 vimeripotiwa. Kufikia sasa watu visa vya uteketejaji wa majengo ya shule vimeshuhudiwa kwenye shule takriban ishirini na tano. Miongoni mwa shule hizo ni ile ya Wasichana ya Buruburu iliyoko Jijini Nairobi, Shule ya Wafulana ya Sigalame, ile ya Kimilili, Ofafa Jericho miongoni mwa nyingine.

Kutokana na hali hii, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri, KUPPET Omboko Milemba alisema ni ishara kwamba wanafunzi wamechoshwa na vipindi virefu vya masomo kwa lengo la kufidia muda uliopotezwa wakati zilipofungwa kutokana na korona na wanahitaji kupumzika.


Madai yanayoibuliwa wanafunzi wanapohusika visa hivi ni kwamba, mfano hawaridhishwi na mwalimu fulani, chakula kibovu na kadhalika. Hata hivyo pia kunayo madai kwamba wengine hufanya hivyo baada ya kuzuia kutazama mechi fulani nakadhalika.

Jingine ni kwamba katika karibu ya kila kisa kinachoripotiwa, mara nyingi mabweni ya shule ndio huteketezwa na ni nadra usikie darasa limeteketezwa ama hata chumba cha maankuli. Ni kutokana na hali hii ambapo Milemba anapendekeza kwamba shule zote za mabweni zibadilishwe ziwe za kutwa. 

Mjadala kuhusu uteketezaji wa majengo ya shule vilevile umeendelea bungeni huku maseneta wakiwamo, Ledama Ole Kina vilevile Seneta Johnson Sakaja wakitaka jamii ijirejelee na kutambua mahali inapokosea katika kuwaelekeza wanafunzi.

Je, anayopendekeza Milemba na washikadau wengine yataleta suluhu katika sekta ya Elimu kuhusu mikasa ya uteketezaji wa majengo ya shule mara kwa mara hali inayowasabishia wazazi mzigo mkubwa kando na ugumu wa maisha

Share this: