×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kamati ya Muungano wa OKA yapinga madai kuhusu Rais kuwashawishi vinara wa muungano huo kumuunga Raila

Kamati ya Muungano wa OKA yapinga madai kuhusu Rais kuwashawishi vinara wa muungano huo kumuunga Raila

Viongozi wa muungano wa OKA wametoa taarifa ya kukanganya kuhusu nia ya mikutano ambayo wamekuwa wakifanya katika Ikulu na kuongozwa na Rais Uhuru Kenyatta huku wakipinga kwamba ni ya kuwashurutisha kuchukua mkondo fulani.

Katika barua iliyoandikwa na Kamati ya Kiufundi, viongozi wa OKA wamevilaumu vuombo vya habari kwa kudai kwamba Rais Uhuuru Kenyatta amekuwa akiwaagiza kufika Ikulu kadhalika kuwalazimu kumuunga mkono Kinara wa ODM, Raila Odinga.

Badala yake, wamesisitiza kwamba mikutano yote imefanywa kwa hiari na maoni ya kila kiongozi kuheshimiwa ikiwa na lengo la kutathmini mustakabali wa taifa. Katika taarifa hiyo pia wamesisitiza kwamba mikakati ya OKA inaongozwa na Kamati ya Kiufundi na Rais Kenyatta hajathubutu kuingilia mikakati hiyo.

Taarifa hii ni kinyume na kauli za viongozi wa OKA wakiongozwa na Kiongozi wa ANC, Musalia Mudavadi ambaye katika baadhi ya mikutano yake ameashiria kuwapo mashinikizo ya kuwapendekeza watu fulani kuwania Urais. Akizungumza wikendi, Mudavadi aliwasisitizia Wakenya haja ya wao kujiamulia wenyewe huku akiapa kutokubali kushinikizwa kumuunga mtu mwingine kuwania Urais.

Kauli hiyo vilevile ilitawala mikutano ya kisiasa ya Naibu wa Rais William Ruto. Ikumbukwe viongozi wa OKA wamekuwa wakikutana na Rais Uhuru Kenyatta mara kwa mara huku mkutano wa hivi punde zaidi ukifanyika Jumamosi, siku moja baada ya muungano wa OKA kuzindua kampeni zake katika Kaunti ya Kakamega.

Share this: