×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais yuko Glasgow-Scotland kwa kongamano la UN

Rais yuko Glasgow-Scotland kwa kongamano la UN

Rais Uhuru Kenyatta atawasili jijini Glasgow, Scotland hapo kesho kwa kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya hali ya anga.

Wakati wa siku ya kwanza ya mazungumzo Rais Kenyatta anatarajiwa kuwaelezea viongozi wengine watakaokuwa katika kongamano hilo kuhusu mikakati Kenya iliyoafikia katika kukabili tatizo hilo.

Licha ya kutohusika katika kuchangia katika madhara ambayo yametokana na mabadiliko ya hali ya anga Kenya i katika mstari wa mbele kuyakabili.

Ikumbukwe Kenya lilikuwa taifa la kwanza Afrika kupitisha sheria kuhusu mabadiliko ya hali ya anga mwaka 2016 ambapo ilikubaliana kwamba asilimia 90 ya umeme unaotumika usiwe na madhara yoyote na inalenga kuafikia asilimia 100 mwaka 2030.

Jumanne Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kukutana na Rais Kenyatta katika kikao kuhusu uvumbuzi.

Aidha bingwa wa mbio za Marathon Eliud Kipchoge atajiunga na Rais Kenyatta katika kampeni ya kuilinda misitu. Mwnariadha huyo aidha amekuwa katika mstari wa mbele katika uhifadhi wa misitu nchini na hata amechukua jukumu la kulinda hekari hamsini katika msitu wa Kaptagat.

Kenya na Uingereza zimekuwa zikishirikaina katika shughuli mbalimbali za kukabili mabadiliko ya hali ya anga. Katika kipindi cha miaka mitatau iliyopita Kenya imepokea ufadhili wa shilingi bilioni 22  katika miradi mbalimbali ya kuimarisha mazingira.

Maafisa wengine watakaoandamana na rais Kenyatta ni Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko na Ukur Yattani wa fedha.

Viongozi wa mataifa mia mbili kote duniani wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo.

Share this: