×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Msitutishe na dola-maslahi-System, asema Ruto

Msitutishe na dola-maslahi-System, asema Ruto

Naibu wa Rais, William Ruto amesikitishwa na jinsi viongozi wa Muungano wa One Kenya Alliance, OKA wanavyoshurutishwa kumuunga mkono Kinara wa ODM, Raila Odinga kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Akihutubu katika eneo la Loitoktok, Kaunti ya Kajiado Ruto amesema demokrasia inazidi kukandamizwa na dola-maslahi yaani System kwa manufaa ya Odinga. Kwa mujibu wa Ruto, Wakenya wana haki ya kumchagua kiongozi wanayempendelea kuambatana na sera zake.

Naye aliyekuwa Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Aden Duale amesema ni Rais Uhuru Kenyatta ndiye anawashurutisha vigogo hao. Kauli yake imetiliwa mkazo na Mbunge wa Mathira, Rigathi Gachagua.

Viongozi wengine walioandamana na Ruto wakiwamo wabunge Peris Tobiko wa Kajiado Mashariki na George Ole Sunkuiya wa Kajiado Magharibi wameendelea kumpigia debe katika azma yake ya kuwania urais. Wawili hao wamemtaka Odinga kutangaza wazi kwamba atakubali matokeo ya uchaguzi mkuu ujao.

Kesho Jumatatu, Ruto ataelekeza kampeni zake katika Kaunti ya Nyamira ambapo ataendeleza misururu ya mikutano kutangaza sera zake za kuwainua Wakenya wenye kipato cha chini.

Ziara ya Ruto Nyamira inajiri wiki moja tu baada ya ile ya Kinara wa ODM Raila Odinga katika eneo hilo.

Share this: