×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Huduma Namba haina maana; imesema mahakama

Huduma Namba haina maana; imesema mahakama

Mahakama Kuu imeharamisha matumizi ya kadi za Huduma Namba nchini. Katika uamuzi huo, Jaji Jairus Ngaah amesema serikali ilikiuka katiba kwa kuendesha usajiliwa wa huduma namba bila kubaini athari zinazoweza kusababishwa na ukusanyaji wa data za Wakenya.

Katika kesi hiyo iliyokuwa ikiendelea mahakamani, suala la usalama wa data aidha liliibuliwa ambapo serikali ilikosolewa pakubwa kwa kukosa kufafanua jinsi itakabvyoyalinda maelezo ya Wakenya.

Uamuzi huu unajiri wakati ambapo serikali imeendelea kuwahimiza Wakenya kujitokeza na kuchukua kadi hizo. Katika taarifa yake ya hivi karibuni kuhusu Huduma Namba, Msemaji wa Serikali Kanali Mustaafu Cyrus Oguna, alisema jumla ya kadi milioni 2.4 miongoni mwa milioni 5 zilizokuwa tayari kufikia mwezi Mei mwaka huu zilikuwa bado hazijachukuliwa.

Share this: