×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Bingwa wa mbio za mita elfu 5 katika mashindano ya Olimpiki kwa upande wa akina dada, Agnes Tirop ameaga

Bingwa wa mbio za mita elfu 5 katika mashindano ya Olimpiki kwa upande wa akina dada, Agnes Tirop ameaga

Bingwa wa mbio za mita elfu 5 katika mashindano ya Olimpiki kwa upande wa akina dada, Agnes Tirop amepatika amefariki dunia.

Tirop ambaye alishiriki mashindano ya Olimpiki makala ya mwaka 2020 yaliyofanyika mwaka huu Jijini Tokyo Japan amepatikana nyumbani kwake katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Aidha, mwili wake umepatikana ukiwa na majeraha tumboni na shingoni. Inadaiwa kwamba huenda mumewe ndiye aliyetekeleza kitendo hicho kwa kuwa wamekuwa katika mzozo kwa muda sasa. Mumewe Agnes aidha anadaiwa kuonekana nyumbani kwa Agnes saa chache zilizopita kabla ya mwili wake kupatikana. Kufikia sasa mwili wake bado haujaondolewa.

Mwaka 2015 Tirop aliweka historia ya kuwa mwanariadha mchanga zaidi duniani kushiriki mashindano ya Kimataifa ya Riadha yaliyoandaliwa na Shirikisho la Riadha Duniani IAAF, baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza katika mbio za mita elfu tano na kuishindia Kenya dhahabu.

Aidha mwaka 2014, aliibuka mshindi katika mbio hizo Barani Afrika na kuwa mwanaridha mchanga zaidi kufanya hivyo kabla ya mwaka 2017 ambapo aliishindia Kenya nishani ya shaba.

Tirop aliyezaliwa mwaka 1995, alianza kung'aa katika riadha mwaka 2012 alipomaliza katika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Kitaifa ya Kenya Cross Country Championship.

Aidha, aliweka rekodi ya kuwa mwanariadha wa kike mwenye kasi zaidi katika mbio za mita elfu kumi, akiwa na umri wa miaka 25 pekee. Vilevile aliweka historia katika mashindano ya mbio za mita elfu tano Jijini Herzogenaurach, Ujerumani akitumia dakika 30.01.

 

Share this: