×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Idara ya Polisi yazindua mpango wa kukabili dhuluma za kijinsia

Idara ya Polisi yazindua mpango wa kukabili dhuluma za kijinsia

Ni afueni kwa waathiriwa wa dhulma za kijinsia, Gender Based Violence baada ya serikali kuzindia mradi wa kushughulikia dhulma hizo, kwa jina Policare.

Akihutubu wakati wa uzinduzi huo, mkewe Rais Uhuru Kenyatta, Margaret Kenyatta amesema kwamba mradi uo utachangia pakubwa kusuluhishwa kwa kesi na visa vya dhulma zinazoripotiwa kutokana na dhulma za kinyumbani kukiwemo ukeketaji.

Aidha, Margaret amesema kwamba mradi huo vilevile unalenga kuwapa afueni waathiriwa kwani mbali na kupata haki, wataweza kutibiwa na kupewa ushauri nasaha.

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Dkt. Fred Matiang'i ambaye pia alikuwepo wakati wa uzinduzi huo uliofanyika hapa Jijini Nairobi, ameupongeza akisema kwamba utachangia pakubwa kufanikisha uchunguzi dhidi ya visa hivyo ambavyo vimeendelea kukithiri nchini.

Share this: