×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Peris Tobiko ajiunga na kambi ya Ruto, mumewe akilia

Peris Tobiko ajiunga na kambi ya Ruto, mumewe akilia

Naibu wa Rais, William Ruto anaendelea kuwapokea wabunge waasi wa Chama cha Jubilee, leo hii akimpokea rasmi Mbunge wa Kajiado Mashariki, Peris Tobiko.

Ruto ameahidi kushirikiana naye, akimsifia kutokana na miradi ya maendeleo katika eneo bunge lake. Kadhalika amekariri kwamba mchujo utafanywa ili kumchagua atakayepeperusha bendera ya UDA hasa ikizingatiwa viongozi wengi akiwamo Mbunge wa Kajiado Kusini, Kato Ole Metito wametangaza azma yao.

Tobiko ambaye amejiunga rasmi na Chama cha UDA ametangaza kuwania ugavana wa Kaunti ya Kajiado, akilenga kumng'atua gavana wa sasa Joseph Ole Lenku.

Tobiko ambaye amezungumza huku akilengwalengwa na machozi amemshukuru Ruto kwa kumkubali katika UDA. Ameelezea haja ya siasa za maendeleo akisema ni za manufaa kwa wananchi.

Viongozi waliohudhuria hafla ya kumkaribisha Tobiko katika UDA nao wameahidi kushirikiana naye huku wakimtaka kuwa tayari kulimbikiziwa sakata za ufisadi na kukamatwa mara kwa mara. Miongoni mwa viongozi hao ni Kimani Ichung'wa wa Kikuyu na Rigathi Gachagua wa Mathira.

Wakati uo huo, Ruto amesisitiza haja ya viongozi kuchaguliwa kutegemea sera zao wala si siasa za chuki. Kauli yake imetiliwa mkazo na Gachagua ambaye amesema ushindani utakuwa baina ya Ruto na Kinara wa ODM, Raila Odinga.

Mkutano huo umefanywa nyumbani kwa Peris Tobiko katika eneo la Ilpolosat. Mkutano huo umemghadhabisha mumewe Tobiko, Kishanto Ole Suuji ambaye amelazimika kumshtaki mkewe kwa madai ya kutoshauriana naye.

Hata hivyo, polisi wamemwarifu kwamba Tobiko ana kibali cha kufanya mkutano nyumbani kwake kwani alikuwa amewaarifu kuhusu ujio wa Ruto.

Share this: