×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Odinga awataka vijana kujisajili kuwa wapigakura

Odinga awataka vijana kujisajili kuwa wapigakura

Kinara wa ODM Raila Odinga amesikitishwa na idadi ndogo ya Wakenya wanaojitokeza kusajiliwa kuwa wapigakura wakiwamo wa maeneo ya Nyanza na Magharibi, ambako ana ufuasi wake mkubwa.

Akizungumza kwenye eneo la Nyando, Raila ambaye anapanga kutangaza rasmi azma yake ya kuwania urais, hajaridhishwa na desturi ya wafuasi wake kuonekana wakipuuza haja ya kuwa na kura.

Katika maeneo aliyoyazuru kwenye kaunti za Vmaafisa wa IEBC katika vituo vingi kwenye kaunti za Vihiga na wameonekana wakiwa wamekaa bila shughuli ya kufanya 

Raila amewahimiza viongozi na maafisa wa chama cha ODM kuwahamasiha wananchi kuhusu umuhimu wa kura.

Kiongozi huyo wa upinzani amesema inasikitisha kwamba wafuasi wake hawajitokezi kwa wingi kama wale wa wapinzani wake.

Shughuli za usajili wa wapigakura itaendelea ndani ya siku thelathini baada ya kuanza tarehe 4 mwezi huu wa Oktoba.

Share this: