×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Magoha azionya shule kuhusu matozo mbalimbali

Magoha azionya shule kuhusu matozo mbalimbali

Walimu wakuu wa shule za msingi wameagizwa kusitisha mara moja malipo wanayotozwa wanafunzi kugharimia mitihani inayoratibiwa na shule.

Akifika mbele ya Kamati ya Elimu katika Bunge la Kitaifa, Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha ametaja matozo hayo kuwa kinyume na sheria.

Kulingana na Waziri Magoha, serikali inagharimia mitihani hiyo kila mwaka hivyo walimu wanaoshinikiza malipo zaidi wanapaswa kukabiliwa kisheria.

Hata hivyo, Magoha ameilaumu Tume ya Huduma za Walimu, TSC kwa kusalia kimya, walimu wakiwapunja wazazi pesa.

Amesema ametoa takribani maagizo thelathini ilhali hakuna hatua zimechukuliwa dhidi ya wahusika. Chini ya mpango mzima wa masomo bila malipo, Magoha amesema serikali inatoa shilingi elfu moja mia nne ishirini kwa kila mwanafunzi, kila mwaka katika shule za msingi za umma.

Amesema pesa hizo hutumwa moja kwa moja katika akaunti za shule, akidokeza kuwa asilimia 50 ya fedha hizo hutolewa muhula wa kwanza, asilimia 30 muhula wa pili, na asilimia 50 nyingine katika muhula wa tatu.

Wakati uo huo, Magoha ametoa agizo la kuadhibiwa kwa walimu wakuu wanaowatuma nyumbani wanafunzi hususan wanaotoka familia maskini kuleta karo.

Share this: