×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wana Mt.Kenya Foundation wamshambulia Ruto na wandani wake

Wana Mt.Kenya Foundation wamshambulia Ruto na wandani wake

Wafanyabiashara wa Muungano wa Mt Kenya Foundation, MKF wamemshambulia Naibu wa Rais William Ruto na wandani wake kwa kutangaza uwezo wao wa kifedha.

Katika kikao na vigogo wa OKA hapa Nairobi, wafanyabiashara hao wamedai kwamba fedha walizonazo zinatokana na bidii na juhudi zao za kila siku na wala si kupitia ufisadi jinsi ilivyo kwa viongozi wengine.

Mwenyekiti wa MKF Peter Munga aidha amedai kwamba ajenda kuu ya viongozi hao ni kuendeleza siasa za kuwachochea Wakenya kwa kuwagawanya katika makundi ya walio na mali na wasiokuwa nayo, akisema ni hatari kwa umoja wa taifa.

Viongozi wa OKA wakiongozwa na Musdalia Mudavadi wa ANC, Kalonzo Musyoka wa Wiper, Gideon Moi wa KANU vilevile Moses Wetangula wamewahakikishia wakazi wa Mlima Kenya kwamba sera zao za uongozi zinajali maslahi ya eneo hilo, yakiwamo kuimarisha sekta ya Kilimo, vilevile mazingira bora ya kufanyabiashara.

Aidha, wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wakazi waeneo la Mlima Kenya waliozungumza wahimiza kuwapo kwa umoja miongoni mwao na kuhanikisha kwamba watakayemuunga mkono anashinda uchaguzi mkuu ujao. Purity Ngunjiri amewawakilisha wanawake katika kikao hicho.

Sawa na ilivyofanyika kwa Kinara wa ODM Raila Odinga, mkutano wa leo sasa unamaanisha kwamba viongozi wa OKA wamepewa idhini ya kutembea eneo la Mlima Kenya na kuomba kura.

Share this: