×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenyapower ni mradi maalumu wa serikali

Kenyapower ni mradi maalumu wa serikali

Serikali imetaja Kampuni ya Kusambaza Umeme, Kenya Power kuwa mradi wake maalumu.

Katika taarifa, Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Dakta Fred Matiang'i amesema hatua hiyo imechukuliwa ili juhudi zote ziwekwe katika kuiboresha kampuni hiyo ambayo inapitia changamoto nyingi.

Kwa mujibu wa Matiang'i, serikali inalenga kurejesha hadhi ya Kenya Power kwani Wakenya wameanza kupoteza imani nayo, baadhi wakikumbatia mbinu mbadala za kupata umeme.

Tangazo hilo linajiri huku maafisa katika kampuni hiyo na wale wa Wizara ya Kawi wakitarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa pamoja.

Matiang'i amedokeza kwamba makachero wa Idara ya Upelelezi, DCI wale Ukaguzi wa Fedha, Mamlaka Mamlaka ya Kurejesha Mali Inayomilikiwa Kinyume na Sheria, Asset Recovery Authority ARA wamejukumiwa kuchunguza ni kwa nini Kenya Power imekuwa ikiandikisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Maafisa hao wameagizwa kuwafanyia ukaguzi maafisa wa mauzo, wafanyabiashara wanaohudumu katika Kenya Power vilevile kuchunguza iwapo kuna mwingiliano wa majukumu, conflict of interest na iwapo kuna maafisa wa kampuni hiyo wanaoshirikiana na mawakala kuitapeli kampuni hiyo.

Wakati uo huo, Matiang'i aliyejukumiwa na Rais Uhuru Kenyatta kusimamia kamati za utekelezaji wa miradi ya serikali, ametoa hakikisho kwamba maafisa watakaopatikana na hatia wataadhibiwa.

Matiang'i amekariri haja ya taasisi zote za serikali kuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma kwa umma bila miingilio ya kisiasa.

Amesema Kenya Power imeingizwa siasa ambazo zinatishia kuisambaratisha kabisa iwapo hatua hazitachukuliwa.

Share this: