×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto awasuta mahasimu wake kwa kukosa ajenda

Ruto awasuta mahasimu wake kwa kukosa ajenda

Naibu wa Rais William Ruto amewashauri mahasimu wa kisiasa kuja na mbinu mwafaka za kuwavutia Wakenya badala ya kuendelea kumkashifu.

Kulingana na Ruto ni wazi kwamba wapinzani wake wamepoteza mwelekeo na wanaendelea kujadili ajenda za Chama cha UDA badala ya kuwashawishi Wakenya kuwaunga mkono.

Akizungumza mjini Kiligoris katika Kaunti ya Narok, Ruto amewasuta mahasimu hao akisema kwamba lengo lao ni kumwangusha.

Ruto amesisitiza kwamba hatishiki na kubuniwa kwa miungano mbalimbali dhidi yake akisema haiwezi kufaulu kwa kuwa ni ya kikabila.

Vilevile, amewakejeli viongozi wa miungano hiyo kwa kushindwa kutangaza wagombea wake wa urais kufikia sasa.

Ruto ameandamana na Wabunge mbalimbali wakiwamo Aden Duale wa Garissa mjini, Kimani Ichungwa wa Kikuyu, wa Mathiria Righathi Gachagua, wa Narok Magharibi Gabriel Tongoyo,  Johna Ng'eno wa Emurua Dikirr na Soipan Tuya miongoni mwa wengine.

Share this: