×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Etale awashauri Wakenya kusajiliwa kuwa wapigakura

Etale awashauri Wakenya kusajiliwa kuwa wapigakura

Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Chama cha ODM, Philip Etale amewashauri Wakenya kutumia muda uliowekwa na Tume na Uchaguzi IEBC kujisajiliwa kuwa wapigakura.

Etale amesema vijana ndio sehemu kubwa ya idadi ya watu nchini hivyo basi wanastahili kushirikishwa pakubwa katika masuala ya uongozi kupitia upigaji wa kura.

Akizungumza na Radio Maisha, Etale amewashauri kutosubiri hadi nyakati za mwisho wa shughuli hiyo kabla ya kujitokeza kusajiliwa. 

Etale ambaye ametangaza azma ya kuwania kiti cha ubunge wa Lugari katika uchaguzi wa mwaka ujao, amewahimiza vijana kuchukua vitambulisho vyao kwenye ofisi za usajili wa watu ili kufanya maamuzi ya busara mwaka ujao.

Kauli yake inajiri huku maafisa wa usajili wa watu nchini wakiendelea kulalamikia idadi kubwa ya watu ambao hawajafika kuchukua vitambulisho vyao.

Share this: